918. LUSHIGU LUMO LUDAB´OJAGA MHULI.

Imhuli ili ndimu nhale noyi iyo yibhakilile abhana ndimi bhichayo. Indimu yiniyo, nulu igacha idub´ola ukulushigu ulumo duhu, kunguno ya bhutale bhoyo bhunubho. Iyoyi ulu yucha mpaga ishigu jikwile, huna yub’ola lulu. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “lushigu lumo ludab´ojaga Mhuli.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na wiyumilija bho gugamala wangu amakoye gakwe, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’winuyo, agabhutumilaga uwiyumilija bhokwe bhunubho, bho gwikala nzala ulu ogayiyagwa ijiliwa ja gulya ulu ulushugu lunulo, kunguno adadulile ugunanuka bho gukija gulya kulushigu lumo duhu. Uweyi agabhambilijaga na bhiye ugugamala wangu amakoye gabho genayo, kunguno ya wiyumilija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni Mhuli iyo idabhojiyagwa na lushugu lumo duhu, ulu yachaga, kunguno nuweyi adabhulagagwa ni nikoye lya lushigu lumo duhu, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “lushigu lumo lugab’ojaga Mhuli.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gugamala wangu amakoye gabho, kugiki bhadule gwiyambilija ugulishigila ilikanza lya guyeja chiza na bhichabho, umuwikaji bhobho.

Waebrania 6:15.

Yakobo 5:7-8.

2 Petro 3:9.

1 Samweli 28:20.

KISWAHILI: SIKU MOJA HAIOZESHI TEMBO.

Tembo ni mnyama mkubwa kuwapita wanyama wenzake. Mnyama huyo, hata akifa haozi kwa siku moja kwa sababu  ya ukubwa wake huo. Yeye akifa huchukua siku nyingi mpaka kuifikia hali hiyo ya kuoza. Ndiyo maana watu husema kwamba, “siku moja haiozeshi tembo.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana uvumilivu wa kuyamaliza haraka matatizo yake, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia uvumilivu wake huo kila anapokosa chakula siku hiyo, kwa sababu anaelewa kwamba hawezi kufa kwa njaa ya kushinda bila kula kwa siku moja tu. Yeye huwasaidia na wenzake katika kuyawaliza haraka matatizo yao, kwa kuutumia vizuri utumilivu wake huo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na Tembo aliyekufa ambaye hawezi kuoza kwa siku moja tu, kwa sababu naye hauliwi na tatizo la siku moja tu, maishani mwake. Ndiyo maana huwaambia watu kwamba, “siku moja haiozeshi tembo.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuyamaliza kwa haraka matatizo yao, ili waweze kusaidiana kuifikia hali ya kufurahi vizuri, maishani mwao.

Waebrania 6:15. “Naye baada ya kungoja kwa saburi, Abrahamu alipokea kile kilichoahidiwa.”

Yakobo 5:7-8. “Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja Kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho. Ninyi nanyi vumilieni tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.”

2 Petro 3:9. “Bwana hakawii kuitimiza ahadi Yake kama watu wengine wanavyodhani kukawia, bali Yeye anawavumilia, maana hataki mtu ye yote aangamie, bali kila mmoja afikilie toba.”

1 Samweli 28:20. “Papo hapo Sauli akaanguka chini akajinyoosha, akiwa amejawa na hofu kwa ajili ya maneno ya Samweli. Nguvu zake zikamwishia kwa maana alikuwa hajala cho chote mchana ule wote na usiku.”

elephant-1-2

elephant-1-

elephant-1-1

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.