Ugulala ng’waje ili gwikala mpaga bhugela ubhujiku bho nduhu unyango a ha numba yiniyo. Inumba yiniyo yigabhizaga idina jihangijo ija gunhemeja munhu ugwingila umukaya yiniyo kunguno ya gwikala ili ng’waje bhujiku pe chiniko. Hunagwene abhanhu abhaha kaya yiniyo bhagacholaga nzila ja gulyinja ilikoye linilo ilya “gulala ng’waje.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhadina jiliwa umukaya yabho. Abhanhu bhenabho, bhagagayiyagwa ijiliwa jinijo ulu mbula yukija ugutula chiza ung’waka gunuyo. Abhoyi bhagakoyiyagwa na nzala nhale kunguno ya gubhiza bhadina jiliwa umukaya jabho.
Abhanhu bhenabho, bhagikola na bhanhu abho bhikalaga bhujiku pe bhadina nyango umunumba jabho, kunguno nabhoyi bhagikalaga ng’waje bho nduhu ugulya ijiliwa umunda jabho. Abhoyi bhagacholaga jiliwa ja kupilila inzala yiniyo. Hunagwene bhagayombaga giki bhali na nzala ya “gulala ng’waje.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gutumama milimo ya mbika ningi iyo idulile gubhapandikala jiliwa ahi kanza lya nduhu mbula, kugiki bhakije ugukonyiwa ni nzala, umuwikaji bhobho.
Mwanzo 26:1.
Mwanzo 41:17 – 36.
1Wafalme 18: 3 – 6.
KISWAHILI: KULALA WAZI.
Hali ya kulala wazi ni ile ya kuishi usiku kucha kwenye nyumba bila kuwa na mlango wa kufungia. Nyumba hiyo, huwa haina kizuizi cha kumzuia mtu kuingia ndani yake, kwa sababu ya kukaa wazi usiku kucha hivyo. Ndiyo maana watu wa kwenye familia hiyo, hutafuta njia za kulitatulia tatizo hilo la “kulala wazi.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao hawana chakula ndani ya familiya yao. Watu hao, hukumbwa na tatizo hilo la kukosa chakula hicho ikikosekana mvua ya kutosha mwaka huo. Wao husumbuliwa na njaa kubwa kwa sababu ya kushindwa kupata chakula hicho kwenye nyumba yao.
Watu hao, hufanana na wale watu waliokuwa wakiishi usiku kucha bila kuwa na mlango wa kufungia kwenye nyumba yao, kwa sababu nao huishi bila kuwa na chakula kwenye matumbo yao. Wao hutafuta njia za kulitatulia tatizo hilo la njaza. Ndiyo maana huweka wazi kwamba, wana tatizo la “kulala wazi.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kufanya kazi za aina mbalimbali zinazoweza kuwapatia chakula wakati wa kipindi cha kukosa mvua, ili wasikumbwe na tatizo la njaa, maishani mwao.
Mwanzo 26:1.
Mwanzo 41:17 – 36.
1Wafalme 18: 3 – 6.
ENGLISH: TO SLEEP IN A DOOR OPEN HOUSE.
This proverb expresses a situation of a person who sleeps in a house which its door is open. A door open house sleeping situation is that of staying all the night in a house that is without a closed door. This house, however, has no barrier to prevent anyone from entering it, because it stays open all night. That is why members of the family are looking for ways to solve this problem because they do not like “to sleep in a door open house.”
This proverb is compared to those who have no food in their family. These people suffer from malnutrition if there is no enough rain in that year. They suffer from severe hunger because they cannot find food in their home.
These people are like those people who stayed the whole night without closing their door, because they also live without food in their stomachs. They look for solutions to the problem of hunger. That is why they make it clear that they have a problem, because they do not like “to sleep in a door open house.”
This proverb imparts in people an idea on how to be patient enough to do various kinds of works that can provide them with food during the dry season, so that they do not suffer from hunger in their lives.
Genesis 26: 1.
Genesis 41:17 – 36.
1Kings 18: 3-6.