866. KALAGU – KIZE. LYAGWINGILA NHAMBO MPAGA LYAGAGWA – LIMI.

Ikalagu yiniyo, ihoyelile higulya ya Limi. Ilimi ligab’izaga guti giki lilipela nhambo gufumila dilu mpaga lyagagwa kwikanza lya mhindi. Ilyoyi lidimaga nulu hadoo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki “lyagwingila nhambo mpaga lyagagwa – Limi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumama milimo yakwe chiza bhuli lushuku, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga guidilila bho guitumama chiza imilimo yakwe yiniyo mpaga oimala chiza. Uweyi agandikaga matwajo mingi umubhutumami bhokwe  bhunubho, kunguno ya bhukamu bhokwe bhunubho ubho gudilila guitumama milimo yakwe mpaga oimala chiza, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agiikolaga ni Limi ilo lidimaga umubhutumami bholyo, kunguno nu weyi agigulambijaga uguitumama imilimo yakwe mpaga oimala chiza bho nduhu uguilekanija. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “lyagwingila nhambo mpaga lyagagwa – Limi.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya guidilila imilimo yabho bho gwigulambija guitumama chiza mpaga bhaimale, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Wagalatia 6:9.

Luka 9:62.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

HUONDOKA KWA MBIO HADI MACHWEO – JUA.

Kitendawili hicho, huongelea juu ya Jua. Jua hilo, huonekana kama kwamba, linakimbia kwa mbio kuanzia asubuhi hadi jioni au machweo yake. Lenyewe huwa halisimami hata kidogo katika utekelezaji wa majukumu yake. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “huondoka kwa mbio hadi machweo – Jua.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake vizuri kila siku, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kuzijali kazi zake kwa kuzitekeleza vizuri mpaga anazimaliza. Yeye hupata mafanikio mengi katika majukumu yake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kujali kufanya kazi zake mpaga anazimaliza vizuri, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana  na Jua lisilosimama kutekeleza majukumu yake, kwa sababu naye hujibidisha kuyatekeleza majukumu yake mpaga anayamaliza vizuri bila kuyatelekeza. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “huondoka kwa mbio hadi machweo – Jua.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujali kazi zao kwa kujibidisha kuzitekeleza vizuri mpaga wazimalize, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Wagalatia 6:9.

Luka 9:62.

 

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.