1495. UDUDUMIJA NONI YA NG’WILAGO BUJIKU WILAGA.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile noni iyo igitanagwa mbilibili. Inoni yiniyo ing’hangala iningi itogilwe gwikala mumalago. Ulu jegela jiduku igabhizaga ulila nakalile ka kagududumija giti ilimuminzi. Giko lulu igabizaga jimanyikijo ja giki ihaha jashiga jidiku ja gandwa gulima. Hunagwene abhanhu bhagayiwilaga giki, “ududumija noni ya ng’wilago bujiku wilaga.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina witegeleja bho gubheja jitumamilo jakwe chiza ulu jegela ijiduku, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, agibhegelajaga ulu jegela ijiduku bho gubheja jitumamilo guti magembe, mapanga ga gusengela malale na gwandya gulima kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho umuwikaji bhokwe. Uweyi agalimaga bho gutumamila jitumamilo jakwe chiza mpaga opandika matwajo mingi aha kaya yakwe yiniyo kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga ni noni iyo igalilaga ulu jegela ijiduku, kunguno nuweyi ulu jegela ijiduku agajibhejaga chiza ijitumamilo jakwe mpaga olima chiza na gupandika sabho ningi ha kaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ududumija noni ya ng’wilago bujiku wilaga.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gubheja pye jitumamilo ja milimo yabho ulu lyegela ilikanza lya kuyitumama imilimo yabho yiniyo, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mwanzo 8:22.

Zaburi 102:13.

Mhubiri 3:1.

Danieli 2:21.

Matendo 1:7.

KISWAHILI: LIA NDEGE WA ENEO LA KABIRU NA MTO, USIKU UMEINGIA.

Chanzo cha msemo huo huongelea ndege anayeitwa dudumizi. Ndege huyo, hupendelea kuishi karibu na mto. Masika jakikaribia, yeye hulia kama yuko majini. Hivyo basi, yeye huwa ni ishara ya kuonesha kwamba kipindi cha kilimo kimekaribia. Ndiyo maana watu humwambia ndege huyo kwamba, “lia ndege wa eneo la karibu na mto, usiku umeingia.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana umakini wa kuandaa vitendea kazi vyake vizuri yanapokaribia masika, katika maisha yake. Mtu huyo, kikikaribia kipindi cha masika huviandaa vitendea kazi vyake vizuri, kama vile majembe, mapanga ya kufyekea maeneo na kuanza kulima, kwa sababu ya umakini wake huo, maishani mwake. Yeye hulima kwa kutumia vitendea kazi vyake vizuri mpaka anapata mafanikio makubwa kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya umakini wake huo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule ndege anayelia kinapokaribia kipindi cha masika, kwa sababu naye kikikaribia kipindi cha masika hujiviandaa vyema vitendea kazi vyake mpaka analima vizuri na kupata mali nyingi kwenye familia yake, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “lia ndege wa eneo la karibu na mto, usiku umeingia.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuviandaa vyema vitendea kazi vyao vyote kinapokaribia kipindi cha kuanza kuzitekeleza kazi zao hizo, ili waweze kupata mafanikio mengi katika familia zao hizo, maishani mwao.

Mwanzo 8:22.

Zaburi 102:13.

Mhubiri 3:1.

Danieli 2:21.

Matendo 1:7.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.