SWAHILI: KOSEA KULENGA MNYAMA MAWINDONI, USIKOSEE KUOA.
Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya mwanamke katika mila za Kiafrika. Hili lilinifanya niwe na utafiti wa kina kwenye kabila la Wasukuma, ambapo wazee wa Wakisukuma (takribani 12) walithibitisha kwamba, ili familia ifanikiwe, jukumu la mwanamke haliepukiki. Kwa hivyo miongoni mwa Wasukuma, mwanamke katika familia anachukuliwa kuwa msaidizi wa karibu wa mumewe katika utunzaji na uhandisi wa shughuli zote za nyumbani.
Kwa hiyo wanaume wa Kisukuma hutumia methali hii “Fujaga ndimu, utize’ fuja nho-la.” Ili kutoa ufahamu kwa vijana wa kiume na wa kike kabla ya kupambanua kuingia katika maisha ya familia.
Methali hii ya Wasukuma inaonesha utimilifu mkubwa wa mwanaume na mwanamke katika familia yao, ikimaanisha kuwa mwanaume anapooa mwanamke shupavu, mwenye moyo mzuri, mwenye nidhamu, Wasukuma huamini kuwa familia nzima itafanikiwa kwa sababu mwanamke na mwanaume wanaweza kusaidiana vizuri katika maisha ya familia
Hivyo basi, wanawake wanapaswa kuelewa kwamba, wana nafasi au wajibu mkubwa wa kutekeleza katika familia zao. Wanapaswa kufurahishwa na hali yao kama wanawake katika familia na jamii zao.
Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, si vema huyo mtu awe peke yake; nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
Marko 10:6-8 “…Mungu akamfanya mume na mke, kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
Waefeso 5:31 “Lakini kila mmoja wenu ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe; na mke na amheshimu mumewe.
ENGLISH: MISS A TARGET WHEN HUNTING, RATHER THAN MARRYING A WRONG WOMAN.
There has been a great discussion on the role of women in the African traditions. This made me have a serious search on the Sukuma Ethnic group, where the Sukuma elders (about 12) confirmed that, in order for the family to prosper, the role of a woman is inevitable. Thus among the Sukuma, a woman in a family is regarded as the closer helper of her husband in keeping and engineering of all domestic activities. Hence the Sukuma men use this proverb “Fujaga ndimu, utize’ fuja nho–la.” So as to give awareness to young men and women before discerning to enter family life.
This Sukuma proverb shows the great complementarity of man and woman in their family, meaning that when a man marries a strong, good hearted, disciplined woman, the Sukuma believe that the whole family will be prosperous because the woman and man can really help each other in family life
Hence, women should understand that, have a great role or duty to perform in their families. They should be happy with their status as women in their family and society.
Gen 2:18 “Then the Lord God said, it is not good that the man should be alone; I will make him a helper fit for him.”
Mk 10:6-8 “….God made the male and female, for this reason a man shall leave his father and mother and be joined to his wife, and the two shall become one flesh…”
Eph 5:31 “however, let each one of you love his wife as himself, and let the wife see that she respects her husband.”


