914. MBITI YALUNDA MAGADO.

Imbiti ilishinu iyo itina bhunwani na bhasabhi bha mitugo, kunguno igabhasolelaga imitugo jabho jinijo. Iyoyi igalundaga magado ayo gali madeni ga mitugo ijo yajisola ukubhasab’i bha mitugo bhenabho.

Giko lulu, bhuli nsab’i ulu wigwa giki ng’wiye osolelagwa ntugo ni mbiti agakolagwa giti osolelagwa weyi, kunguno nuweyi nulu ng’wiye oli osolelwa ntugo ni lib’iti linilo.

Kuyiniyo lulu, b’uli kaya iyo ilina mitugo idaitogagwa imbiti yiniyo, kunguno yokaja magado (madeni) ayo idagashoshaga. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “mbiti yalunda magado.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agasolaga ginhu aliyomba giki agujishosha na oleka ugujishosha. Umunhu ng’wunuyo, agasolaga jikolo ja bhiye jinijo guti alilanda, ulu winhiwa naojikalana duhu. Uweyi agamanyikaga ukubhiye kunguno ya gukija ugubhashokeja ijikola jabho jinijo ijo ojisola, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni mbiti iyo yokaja madeni ga mitugo ja bhanhu, kunguno nuweyi agikalaga na jikolo ja bhanhu bhingi ijo adajishoshaga, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “mbiti yalunda magado.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na nhungwa ja gushosha ijikolo ijo bhab’asoja abhichabho, kugiki bhadule gwikala bho nduhu madeni, umuwikaji bhobho.

Yoshua Bin Sira 8: 12.

Mathayo 18: 23-35.

Warumi 13: 8-10.

KISWAHILI: FISI KARUNDIKA MADENI.

Fisi ni mnyama asiyekuwa na urafiki na matajiri wa mifugo, kwa sababu huwachukulia migugo yao. Yeye hurundika madeni anapowachukulia matajiri hao wa mifugo yao hiyo.

Hivyo basi, kila tajiri wa mifugo hiyo, agikisia kwamba fisi amechukua mfugo wa mwenye mtu, hukasilika akifikiria kama amechukua mfugo wake, kwa sababu ya kumfikiria fisi huyo kama ndiye aliyekuchukua pia mfugo wake au wa jirani yake.

Kwa hiyo, kila familia yenye mifugo haimpendi fisi huyo, kwa sababu amejaza madeni hayo ya kuwachukulia mifugo yao. Ndiyo maana watu husema kwamba, “fisi amerundika madeni.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huchukua vitu vya wenzake na kukaa navyo bila kuwarudishia. Mtu huyo, huchukua vitu vya wenzake hao kwa njia ya kuazima, halafu wanapompatia anabaki navyo bila kuwarudishia. Yeye hujulikana kwa wenzake hao kwa sababu ya kutowarudishia vitu vyao hivyo, alivyovichukua, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule fisi aliyerundika madeni ya kuchukua mifugo ya watu, kwa sababu naye hawarudishii watu vitu vyao aliwavichukua kwa njia hiyo ya kuazima, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “fisi karundika madeni.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia ya kurudisha vitu vya wenzao, walivyovichukua, ili waweze kuishi bila kuwa na madeni, maishani mwao.

Yoshua Bin Sira 8: 12.

Mathayo 18: 23-35.

Warumi 13: 8-10.

hyena-1

hyena-

ENGLISH: A HYENA HAS ACCUMULATED DEBTS.

Hyenas are not friendly to rich animal care takers, because they steal their animals and run away with them. They accumulate debts by stealing the riches of livestock of these people.

Thus, every wealthy animal owner, who hears that the hyena has taken someone else’s livestock, suspects it and gets angry by thinking that it was the one that took his own livestock. He hunts such animal because he thinks such hyena has also taken his own or his neighbor’s livestock.

Therefore, every family which has livestock does not like the hyena, because it has not paid the debt of taking their livestock. That is why people say that, “a hyena has accumulated debts.”

This proverb is likened to a man who takes his fellow man’s possessions and then stays with them without returning them. This person confiscates the belongings of his colleagues, and when they give them to him, he retains them without returning them. He is known to his fellows for not returning their possessions, which he took from them, in his lifetime.

This man is like the hyena that accumulated debts by taking people’s livestock, because he also does not return the people’s belongings which he took from them in a way of borrowing them, in his life. That is why people say to him that, “a hyena has accumulated debts.”

This proverb teaches people on how to have the habit of returning the things of others, which they took, so that they can live without debt, in their lives.

Joshua Bin Sirach 8:12.

Matthew 18: 23-35.

Romans 13: 8-10.

kruger-

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.