148. NG’OMBE JA NG’WISE JA MALA KUB’USHU – WILULI

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya jigano jinijo ililola linti ilo ligitanagwa wiluli. Ilinti lyenilo ligabyalaga bhana b’ape ukwitindigishi. Giko lulu igalenganijiyagwa na ng’ombe ya mala kub’ushu.

Ijigano jinijo jigalenganijiyagwa nu umukikalile kabhanhu nu mkalangile ka bhabyaji b’ab’o. Ung’wana atiko uguikilila iyo agalangagwa na nhungwa ja bhabyaji bhakwe. Ilichiza abhabyaji bhabhize na nhungwa ja wiza ijikomile gub’alanga chiza abhana. Ilenganilile na lusumo ulo luhayile, “ng’homba yalondela igokola.”

Ijigano jinijo jab’alanga abhanhu higulya ya kub’iza na nhungwa jawiza ijiikomile gub’alanga abhana bhabho bho gub’inha jigemelo jawiza. Giko lulu, ijigano jinijo jab’alanga abhabyaji kub’alela chiza ab’ana b’ab’o na kub’atongela chiza kugiki nab’o bhadule gub’iza na nhungwa jawiza umukikalile kab’o na bhanhu.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA

NG’OMBE ZA KWETU ZINA RANGI USONI – MTI.

Chanzo cha kitendawili hicho kinauangalia mti unaoitwa ‘wiluli” (mti wenye rangi mbalimbali). Mti huo hutoa mbegu nyeupe chini kwenye shina lake. Hivyo basi, mtu huo hulinganishwa na ng’ombe mwenye mabaka meupe usoni.

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa watu hasa wazazi wanavyoishi na kuwafundisha watoto wao. Mtoto hawezi kuwa tofauti na yale afundishwayo na tabia za wazazi wake.

Wazazi wanatakiwa kuwa na tabia njema za kuweza kuwafundisha watoto wao kwa kuiga maisha yao ili waweze nao kuishi vizuri na watu wengine. Kitendawili hicho hufanana na methali isemayo ‘Uji hufuata kiwiko.’

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema iwezayo kuwakuza vyema watoto wao na kuwalea kwa kuwapatia mifano ya kuiga ili waweze kujijengea tabia njema iwezayo kuwaletea maendeleo maishani mwao.

“Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.” (Waefeso 6:1-4).

“Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu na uovu kama kwa kamba za mkokoteni,” (Isaya 5:18).

“Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako.” (Mithali 1:8).

“Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, maarifa badala ya dhahabu safi, kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna cho chote unachohitaji    kinacholingana naye.” (Mithali 8:10-11).

“Ye yote apendaye maonyo hupenda maarifa, bali yeye achukiaye kurekebishwa ni mpumbavu.” (Mithali 12:1).

147. KALAGU – KIZE NIGUMHA HISHIGI B’ALULI B’IDAGUKA – MHANDE

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya jigano jiniji ililola mhande na munhu uyo ajibhuchije. Ulu munhu uyo oub’uchaga mhande mlijiseme wiguumha hishigi, jigwidika aliyo lulu, jigab’izaga na yombo nhale gete.

Ijigano jinijo jigalenganijiyagwa kuli munhu uyo adajilab’ilaga chiza ijikolo jakwe. Agab’izaga adinabho ubhudiliji bho jikolo ijoalijipandika, kulwa nguno ya bhulekanija ubho alinabho.

Ugwigumha ahishigi na gwidika go mhande, jililomela ubhugawiwa bho b’uhuguku ubhogulanghana na gulab’ila chiza isabho ijo alinajo umunhu ng’hunuyo aho alikalila.

 Ijigano jinijo jilib’alanga abhanhu higulya ya kub’iza na b’ulab’iji wiza bho jikolo jabho. Idijichiza ugujilekanija isabho ijob’alinajo.

Kuyiniyo, igelelilwe umunhu ab’ize na bhuhuguku ubho bhukomile gumwambilija ugulanghana ijo alinajo, ijib’izile kihamo na sabho, bhupanga bhokwe, nimo gokwe, b’usuluja bhokwe, na witanwa bho b’utumami bhokwe ubho alinabho.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA

NIMEJIKWAA KWENYE KISIKI AKINALULI WAKAMWAGIKA – NJUGU MAWE

Maana ya kitendawili hiki inaangalia njugu mawe na mtu alizo nazo. Mtu aliyebeba njugu mawe kwenye chombo akijikwaa kwenye kisigi, njugu mawe hizo humwagika na kupiga kelele kabisa.

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa havijali vizuri vitu vyake. Huwa hana utunzaji mzuri wa mali alizonazo kwa sababu ya utelekezaji wa vitu alionao.

Kujikwaa kwenye kisiki na kumwagika kwa njugu mawe hueleza hali hiyo ya kukosa uangalifu wa kutunza mali alizonazo, pale anapoishi.

Hivyo, kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kuwa na utunzaji mzuri wa mali zao. Siyo vizuri kutelekeza hovyo mali wazipatazo.

Kwa hiyo, mtu anatakiwa kuwa na uangalifu uwezao kumsaidia kuzutunza alivyo navyo, ikiwa ni pamoja na mali, maisha yake, kazi yake, biashana yake, na wito wa utumishi alionao.

“Yesu akaendelea kusema: “Kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili. Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Hivyo akawagawia wanawe mali yake. ‘‘Baada ya muda mfupi, yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokwa navyo, akaenda nchi ya mbali na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa.” (Luka 15:11-13).

“Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi pamoja nawe na ndugu zako manabii na wote wanaoyashika maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu!’’ Kisha akaniambia, “Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu wakati umekaribia. Atendaye mabaya na aendelee kutenda mabaya, aliye mchafu na aendelee kuwa mchafu, yeye atendaye haki na aendelee kutenda haki na yeye aliye mtakatifu na aendelee kuwa mtakatifu.’’ “Tazama, naja upesi! nikiwa na mshahara wangu, nami nitamlipa kila mtu sawasawa na alivyotenda.” (Ufunuo 22:9-12).

146. LUKANDO KANDO LO NG’WANA MBATI WISANYA JAKWE

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya kahayile kenako ilinola munhu uyo agikalaga na lukando kando na adakangilwe mhayo gose gose, kulo giki wimanile igiki alinajo ijikolo. Ijikolo jinijo jili giti ng’ombe, hela, malale, na manumba.

Giko lulu, umunhu ng’wunuyo agikalaga wimanile igiki nulu agapandika mayange, nduhu amakoye nguno agwigunana bho jikolo jakwe. Huguha giki, ung’wenuyo wisanije jikolo jakwe umuwikaji bhokwe.

Gashinaga lulu, akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo wisanije jikolo jakwe umuwikaji bhokwe. Ung’wunuyo adakangagwa kulwa nguno ya jikolo jinijo ijo ajisanije.

Akahayile kenako kadulanga higulya ya kuleka inhungwa ija bhudoshi umukikalile kise. Tub’ize na nhungwa jawiza ijagudambilija gwikala nab’umo na b’igisu, kunguno dudina ginhu ijagudosela. Idichiza ugudosela majikolo ga musi ng’wenumu, kunguno gose agenayo galab’ita.

KISWAHILI: KUJIDAI DAI KWA MWANAFURANI ATEGEMEA CHAKE.

Chanzo cha msemo huo kinamwangalia mtu ambaye huwa na tabia ya kujidai maishani mwake. Mtu huyo hatishwi na neno lolote, kwa sababu ya mali zake anazozitegemea. Mali hizo ni kama ng’ombe pesa, mashamba na majumba.

Hivyo basi, mtu huyo huwa anajiamini kwamba, hata kama akipata matatizo, atazitumia mali hizo katika kutatua matatizo hayo. Ndiyo kusema kwamba, mtu huyo hutegemea mali zake maishani mwake. Hujiona yeye kuwa hawezi kuhangaika, kwa vile atatumia mali hizo katika kutatua matatizo hayo.

Kumbe basi, msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye hutumainia mali zake maishani mwake. Mtu huyo huwa hatishwi na kitu kwa sababu ya mali zake hizo anazozitegemea.

Msemo huo hutufundisha juu ya kuacha tabia yenye majivuno ya kuzarau wengine maishani. Badala yake tuwe na tabia njema iwezayo kusaidia katika kuishi maisha yenye umoja na wenzetu, kwa sababu hatuna cha kulingia au kujivunia. Ndiyo kusema kwamba, siyo vizuri kulingia mali za hapa duniani kwa sababu hizo zote zitapita.

“Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki.” (Zaburi 31:18).

“Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka.” (Zaburi 101:5).

“Majivuno ya mwanadamu yatashushwa na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, BWANA peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo, nazo sanamu zitatoweka kabisa.” (Isaya 2:12).

“Basi sikilizeni ninyi msemao, ‘‘Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida.’’ Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. Badala yake, inawapasa kusema, ‘‘Kama Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.’’ Kama ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kwa namna hiyo ni kubaya. Basi mtu ye yote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.” (Yakobo 4:13-17).

“Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi ndani ya wale wasiotii. Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukifuata tamaa za mwili na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine ye yote. Lakini Mungu, kwa upendo Wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema.” (Wafilipi 2:1-5).

145. NENE NADACHAMAGWA UKONALOLILE NAGUSHIKA UKO NALIJA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya kahayile kenako ililola ginhu ijo jidachamagwa guti mongo. Nguno umongo gugajaga mpaga uko guligagelela na gudab’izaga na nchami.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapangaga milimo yake na guidilila chiza ijinaguitumama. Umunhu ng’wunuyo agaginjaga amapinjapinja ayo gakomile gugulemeja ugutumamwa unimo gunuyo. Adina bususanya umub’utumami bho milimo yakwe.

Akahayile kenako kalidulanga higulya ya kuleka gub’iza na b’ususanya. Uluuhaya gulondeja mhayo, ilichiza uje na ngholo yimo.

Ilichiza kumtumamila Sebha Yesu bho ngholo yimo pye ishigu ja wikaji bho musi ng’wenumu. Diyangule gunhondeja weyi bho nduhu gususanya mpaga dupandike ubhupanga ubho bhudashilaga.

KISWAHILI: MIMI SIZUWILIWI NINAKOENDA MPAKA NIFIKE HUKO NINAKOENDA

Maana ya msemo huo inaangalia kitu ambacho hakizuiwiliwi, kwa mfano mto, kwa sababu mto huenda mpaka unakokomea, huwa hauziwiliwi.

Msemo huo hulinganishwa na mtu ambaye hupanga mipango yake na kuifuatilia vizuri katika kuukamilisha utekelezaji wake. Mtu huyo huondoa mapingamizi ya mipango hiyo, kwa vile huamua kufanya kitu hicho bila kusitasita.

Msemo huo hutufundisha juu ya kutokuwa na kazi za kusita sita katika maisha yetu. Ni vizuri kufanya kazi kwa roho moja au kwa bidii bila kusisita.

Ni vizuri kumfuata Bwana Yesu kwa moyo mmoja siku zote za hapa duniani. Tuamue kumfuata Yeye bila kusitasita, mpaka tuupate uzima wa milele.

 “Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka.” (Mathayo 24:13).

“Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni.” (Yohane 16:21).

“Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.” (Ufunuo 2:10).

144. NAB’UNDALAGA NDIHAJIGANGA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Imbuki ya kahayile kenako igayombagwa na munhu uyo wisanije ginhu jakwe ijo ajaminile, nulu munhu uyo obiisha jiliwa jingi. Huyo agayombaga giki ‘nab’undalaga ndihajiganga.’

Giko lulu agwikala amanile igiki aduluhiwa ni nzala, kulwa nguno alinajo ijiganga. Ijiganga jinijo hijiliwa jakwe.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo abizaga na jikolo jileb’e ijo ajisanije gete umuwikaji bhokwe. Ijikolo jinijo jigang’winhaga nhinda ja guigimba umumasala gakwe.

Akahayile kenako kadulanga higulya ya gulekana nayo iyamusi ng’wenumu iyabhubhi. Duhandatile mli Yesu, kulwa nguno ung’wunuyo hii jiganga jise. Duleke ugwisanya ginhu jingi aha bhutongi yakwe UYesu.

KISWAHILI: NIMELALA KIFUDIFUDI KWENYE MWAMBA

Maana ya msemo huo inaangalia mtu anayejivunia kitu mbele yake anacho kiamini, au mtu ambaye alilima mazao yake na akapata mavuno mengi. Mtu huyo husema kwamba, ‘nimelala kifudifudi kwenye mwamba.’

 Hivyo, basi atakaa akijua hivyo kwamba hatateseka na njaa kwa sababu anajivunia mwamba huo alionao ambao ni chakula chake. Hicho ndicho akitegemeacho.

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa na kitu fulani ambacho hukiamini kabisa maishani mwake. Kitu hicho humpa kiburi cha kujigamba katika akili zake.

Msemo huo hutufundisha juu ya kuachana na mambo ya duniani yapinganayo na Mungu. Unatufundisha kumfuata Yesu Kristo peke yake, kwa sababu Yeye ndiye mwamba au nguvu yetu. Tusijivunie mali nyingine mbele yake Yesu Kristo.

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.” (Waefeso 2:8-10).

“Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu Yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki Yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. Alifanya hivyo ili kuonyesha haki Yake wakati huu, ili Yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.” (Waroma 3:25-26).

“Nawaambia tumieni mali ya dunia kujipatia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.” (Luka 16:9).

“Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa na hekima na maneno ya kuwashawishi watu, bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho Mtakatifu ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.” (1Wakorintho 2:4-5).

“Kwa maana katika Injili haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa, haki ile iliyo kwa njia ya imani hadi imani. Kama ilivyoandikwa: ‘‘Mwenye haki ataishi kwa imani.’’” (Waroma 1:17).

143. LUB’UB’U LUGANSHOGELAGA UYOOLUTUMYA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Mbuki ya kahayile kenako ililola lub’ub’u. Ulub’ub’u lugigelaga ulu munhu agushimizaga. Aguyuludundumucha aliyo luguyunshogela nuwei uyo agulutumyaga.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa nu kumiito ga bhanhu, inguno amiito genayo gaganhondejaga bhuli ng’wene uyo agagitaga umuwikaji bhokwe. Ulu munhu wita miito gawiza, agubhiza na bhuyegi, umuwikaji bhokwe. Aliyo ulu miito gakwe gib’iza gabhub’i, gagung’wenhela makoye, umuwikaji bhokwe.

Ukubhanhu akahayile kenako kalilola munhu uyo witaga mihayo ya sagala, nulu giti gwib’a, guyomba b’ulomolomo, bhupondya, na yingi iyoyikolile ni yeniyo. Giko lulu, ulugiki mihayo yudaama, aguimala nu ng’witi oyo.

Akahayile kenako kadulanga higulya ya kulekana ni mihayo iyabhub’ub’i, giti yeniyo iyasagala. Kunguno imihayo yeniyo idulile guduchala ku makoye, umuwikaji bhokwe.

Ijinagongeja, akahayile kenako kadulanga higulya ya kub’iza na nhungwa jawiza, ijagwita miito gawiza, ayogadulile gudenhela b’uyegi bho gwikala na mholele na bhigisu umuwikaji wise.

VUMBI HUMRUDIA ALIYE ITIMUA

Maana ya msemo huo inaangalia vumbi. Vumbi hutokea wakati mtu akitembea. Vumbi hilo humfuata yule anayelitimua.

Msemo huo hulinganishwa na matendo ya watu, kwa sababu matendo hayo humfuata kila mmoja yale aliyoyafanya katika maisha yake. Kama mtu akitenda matendo mema, atakuwa na furaha maishani mwake. Lakini kama matendo yake yatakuwa mabaya, yatamuletea matatizo maishani mwake.

Kwa maana hiyo, msemo huo unamwangalia mtu anayetenda matendo ya hovyo kama vile kuiba, kusema uongo, kubaka na mengine kama hayo. Hivyo basi mambo yakiwa magumu, atayamaliza yeye aliyeyatenda.

Msemo huo hutufundisha juu ya kuacha maneno na matendo ambayo ni ya hovyo kama hayo. Kwa sababu maneno na matendo hayo yatatupeleka kwenye matatizo.

Zaidi ya hayo, msemo huo hutufundisha juu ya kuwa na tabia njema ili matendo yetu yaweze kutuletea furaha ya kupata maendeleo ya kuishi kwa amani na wenzetu maishani mwetu.

“Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu katika ya viungo vya mwili wetu. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanam.” (Yakobo 3:5-6).

“Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, nayo Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria. Wote walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na tamaa zake. Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.” (Wagalatia 5:16-26).

“‘‘Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba, kwa maana lango ni pana na njia ni pana ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa kupitia lango hilo. Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyo ielekayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.’’ “Jihadharini na manabii wa uongo, wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini ndani wao ni mbwa mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? Vivyo hivyo, mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Hivyo, kwa matunda yao, mtawatambua.’’ “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza mingi? Ndipo nitakapowaambia wazi, `’Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’” (Mathayo 7:13-23).

“Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, bali hujidanganya moyoni mwake, dini yake mtu huyo haifai kitu.” (Yakobo 1:26).

142. WENUBHU WILIGAGA NDINHO

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Mbuki ya kahayile kenako ililola munhu uyo alinzugi obhugali, ulu giki ubhugali bhunubho b’udapile. Ubhagali bhunubho bhugab’izaga bhutaganu.

Abhanhu bhagayombaga chene giki ‘ubhunubhu wiligaga ndinho.’ Mumho ubhugali bhunubho b’ulib’ub’isi.

Ukubhanhu akahayile kenako kalolile munhu uyo alitumama nimo bho nduhu gub’iza na bhulingisiji. Adatumamaga bho bhugalili mpaga ogumala.

Akahayile kenako, kakalenganijiyagwa nukubhanhu ijinabhukuji bhobho na bhutumami bhobho.

Ulu munhu ab’iza alingokolo alikola na bhugali ubho wiligile ndinho. Munho ogiliga amalange agagub’iza alintumami nkamu omilimo.

Aliyo ulu munhu ub’iza alintumami nkamu omilimo, mumho wikolile na bhugali ubho bhupile. Ubhunubho bhudagwiligile undinho. Ukwene huguhaya giki, umunhu ng’wunuyo, alangile chiza.

Akahayile kenako kalidulanga higulya ya gutumama milimo yise yose bho chiza, yaya uguja wangu bho nduhu bhulingisiji. Ili chiza ugugutumama unimo bho bhulingisiji bhutale.

Hangi akahayile kenako kalilanga higulya ya gub’iza na nhungwa ja wiza. Inhungwa jinijo jigalenganijiyagwa na bhugali ubho bhupile.

Kuyiniyo lulu, akahayile kenako kalinhugula umunhu uyo agatumamaga nimo bho nduhu gub’iza na bhulingisiji bhutale. Umunhu ng’winuyo, igelelilwe kutumama nimo bho chiza na bhulingisiji bhutale mpaga agumale chiza.

KISWAHILI: HUU UMEUKWEPA MWIKO

Maana ya msemo huo inaangalia mtu anayesonga ugali.  Kama ugali utakuwa laini, na tepetepe, maana yake, ugali huo ni mbichi.

Watu husema kwamba, ‘huo umeukwepa mwiko.’ Maana yake, ugali huo ni mbichi. Huo ni ugali ambao haujaiva.

Kwa watu, msemo huo huangalia mtu anayefanya kazi bila kuwa na umakini. Mtu huyo hafanyi kazi kwa umakini unaotakiwa mpaka kuimaliza.

Msemo huo hulinganishwa na malezi ya mtu katika makuzi yake na utendaji wake wa kazi.

Mtu huyo akiwa mvivu hulingana na ugali ulioukwepa mwiko. Ndiyo kusema, kwamba, mtu kama huyo aliyakwepa malezi yatakiwayo kwa mtu kuwa mfanya kazi mwenye bidii.

Lakini kama mtu huyo ni mwenye bidii katika kufanya kazi, hufanana na ugali ulioiva. Ugali huo haukuukwepa mwiko. Ndiyo kusema, kwamba, mtu huyo ana malezi mema.

Msemo huo hutufundisha juu ya kufanya kazi zetu vizuri na kwa bidii na umakini mkubwa. Ni vizuri kufanya kazi kwa umakini unayotakiwa hadi kuifikisha mwisho wake kwa ajili ya kupata mafanikio mengi na mazuri katika maisha yetu.

Zaidi ya hayo, msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema. Tabia hiyo hulinganishwa na ugali ulioiva vizuri.

Kwa hiyo, msemo huo, humuonya mtu anayefanya kazi bila kufuata utaratibu sahihi unaotakiwa. Mtu huyo anatakiwa kufanya kazi kwa kufuata utaratibu sahihi na kwa bidii ili aweze kuifanya kazi hiyo kwa usahihi mpaka kuimaliza.

“Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka.” (Mathayo 24:13).

“Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana. Iweni na furaha katika tumaini, katika dhiki iweni na saburi, dumuni katika maombi. Changieni katika mahitaji ya watakatifu, wakaribisheni wageni.

 Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.” (Waroma 12:11-15).

“Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.” (Yohana 16:21-22).

“Lakini kufuatana na ahadi Yake, sisi tunatazamia kwa furaha mbingu mpya na dunia mpya, ambayo haki hukaa ndani yake. Kwa sababu hii, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia kwa furaha mambo haya, fanyeni bidii ili awakute katika amani, bila mawaa wala dosari. Nanyi hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni wokovu, kama vile ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima ile aliyopewa na Mungu.” (2Petro 3:13-15).

“Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu.” (Ufunuo 3:19).